Survey Evaluating Project “Nyumba ni Choo”

Project “Nyumba ni Choo” is implemented by Project CLEAR, an organization working to enhance the effectiveness of development efforts in Tanzania. The project specifically aims to improve handwashing and sanitation across Tanzania, with a focus on the fight against coronavirus. It is funded in part by the United Kingdom’s Department for International Development (DFID).

As part of the project, a survey is conducted as part of a research effort whose purpose is to evaluate the effectiveness of an awareness campaign called “Mikono Safi, Tanzania Salama” (“Clean Hands, Tanzania Safe” in Swahili), and conducted by the project. The campaign was implemented in 2020 in Tanzania for the purpose of increasing handwashing in the face of COVID-19. The survey is conducted by the specialized firm Geopoll, and a sample of around 1000 respondents are expected to participate. As part of the research effort, the survey includes six experiments where respondents randomly receive questions that are slightly different, so that the effects of these differences in questions can be assessed. These experiments pertain to the effectiveness of awareness strategies, and the conditions for the spread of false information.

It takes about 15 minutes to respond to the entire survey, and all is done by text, so participation presents no risk to the respondent during or after the survey. To answer questions, respondents send their responses by text, free of telecom charge to them. Responses are kept entirely confidential, and they are de-identified so that the respondent’s answers cannot be tied to their identity. Participation is entirely voluntary, and only respondents who consent by replying that they opt into taking the survey receive the questions. Respondents can stop at any time during the survey by sending ‘STOP’, in which case they immediately stop receiving the survey texts. No benefits to which participants are otherwise entitled are tied to taking the survey, or to completing it. Top-up is made available to participants who complete the survey, and is sent automatically to their phone numbers within two days. All Tanzanians selected into the sample are eligible to participate in the survey as long as they are aged 18 or above, live in mainland Tanzania, and know about coronavirus.

In case of questions about the research or the survey, or if there are any doubts about the comprehension of survey participation, respondents can contact Project CLEAR (projectclear.com/contact, or [email protected]) and Geopoll (geopoll.com/community). If you have any questions regarding your rights as a participant in the study, you may contact Solutions IRB (the body that oversees our protection of study participants) at +18552264472 or [email protected].

Relevant research findings will be disseminated by Project CLEAR, including on the website projectclear.com.

Swahili

Dodoso la Tathmini ya Mradi “Nyumba ni Choo”

Mradi wa “Nyumba ni Choo” unatekelezwa na shirika la Project Clear, ambalo limejikita katika kuongeza ufanisi wa juhudi za maendeleo nchini Tanzania. Mradi huo unakusudia kuendeleza uoshaji wa mikono na usafi wa mazingira nchini, msisitizo ukiwekwa katika vita dhidi ya virusi vya corona. Mradi umefadhiliwa kwa kiasi na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID).

Kama sehemu ya mradi huo, dodoso linafanywa kwa lengo la utafiti, ambao madhumuni yake ni kutathmini ufanisi wa kampeni ya uhamasishaji inayoitwa “Mikono Safi, Tanzania Salama”, na unafanywa na mradi huo. Kampeni hiyo ilitekelezwa mnamo 2020, nchini Tanzania kwa madhumuni ya kuendeleza uoshaji wa mikono kipindi cha coronavirus. Dodoso hilo unafanywa na kampuni bobezi ya Geopoll, na sampuli ya wahojiwa takriban 1000 inatarajiwa kushiriki. Kama sehemu ya utafiti, dodoso hilo lina majaribio sita, ambapo wahojiwa wanapokea maswali ambayo ni tofauti kidogo tukilinganisha na maswali ya wahojiwa wengine, ili athari za tofauti hizi za maswali ziweze kupimwa. Majaribio haya yanahusu ufanisi wa mikakati ya uhamasishaji, na uenezi wa habari za uwongo.

Inachukua takriban dakika 15 kujibu maswali yote ya dodoso, na kila kitu kitafanyika kupitia ujumbe. Ushiriki hauleti athari kwa wahojiwa wala hauwadhuru, wakati wa dodoso au baada yake. Katika kujibu maswali, wahojiwa wanatuma majibu yao kwa ujumbe, bila kutozwa ada/malipo ya simu. Majibu huhifadhiwa kwa usiri, na hayawezi kuunganishwa na utambulisho wa wahojiwa. Ushiriki ni kwa hiari kabisa, na wahojiwa tu ambao wanaochagua kushiriki katika dodoso (kitu ambacho kinafanywa kwa kujibu meseji mwanzoni) ndio wanapokea maswali. Wahojiwa wanaweza kujitoa wakati wowote kwenye dodoso kwa kutuma ‘SIMAMA’, ambapo mara moja wataacha kupokea ujumbe ya dodoso. Hakuna faida ambazo washiriki wanapata kawaida katika maisha na hawatapata kwa kuamua kutoshiriki katika dodoso au kutolimaliza. Wahojiwa wanaomaliza dodoso watapata vocha itakayotumwa moja kwa moja kwenye nambari zao za simu ndani ya siku mbili. Watanzania wote wanaochaguliwa kwenye sampuli wanaweza shiriki kwenye dodoso endapo wana umri wa miaka 18 au zaidi, wanaishi Tanzania bara, na wanajua kuhusu virusi vya corona.

Endapo kuna maswali juu ya utafiti au dodoso, au ikiwa kuna mashaka yoyote juu ya uelewa wa ushiriki katika dodoso, wahojiwa wanaweza kuwasiliana na Project CLEAR (projectclear.com/contact, au [email protected]) na Geopoll (geopoll.com/community). Kama utakuwa na maswali yoyote kuhusu haki zako kama mhojiwa katika utafiti, unaweza kuwasiliana na Solutions IRB (shirika ambalo linasimamia usalama wa wahojiwa wa utafiti, kwa kutumia +18552264472 au [email protected].

Matokeo makuu ya utafiti yatasambazwa na Project CLEAR, pamoja na kwenye tovuti ya projectclear.com.